Baraza la Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (Zanzibar Fair Competition Tribunal – ZFCT) ni mojawapo ya Taasisi iliyoundwa chini ya kifungu cha 26 cha Sheria ya Ushindani Halali wa Biashara na kumlinda Mtumiaji Nambari 5 ya mwaka 2018.
Mwaka 1995, Serikali ilitunga sheria ya kufuta sheria ya kusimamia mwenendo wa biashara na kumlinda Mtumiaji ya Zanzibar Nam.2 ya mwaka 1995, na kutunga sheria mpya ya Ushindani Halali wa Biashara na kumlinda mtumiaji kuweka masharti bora zaidi pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo. Baraza limeanza rasmi mnamo mwishoni mwa mwezi wa Oktoba 2020, baada ya kukamilika kwa uteuzi wa Mwenyekiti, Wajumbe na Mrajis wake.
DIRA
Kuwa Baraza bora la Rufaa katika masuala ya Ushindsni Halali wa Biashara.
DHAMIRA
Kupokea na kutoa maamuzi ya mashauri ya Rufaa
Maadili ya Msingi ya Baraza
Baraza la Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar linafanya kazi kwa kufuata maadili ya msingi yafuatayo:
- Haki kwa wakati unaofaa
- Ufanisi na Tija
- Uadilifu na Heshima
- Usawa na Uhuru
- Ushirikiano
- Uwazi